Uranusi

(Elekezwa kutoka Uranus)


Kuhusu matumizi ya jina Zohali kwa sayari hii tazama kipengele cha "Asili ya jina"

Uranusi
Picha yenye rangi halisi ya Uranusi kama ilivyoonwa na Voyager 2 mnamo 22 Januari 1986.
Picha yenye rangi halisi ya Uranusi kama ilivyoonwa na Voyager 2 mnamo 22 Januari 1986.
Ugunduzi
MgunduziWilliam Herschel
Tarehe13 Machi 1781
Jina
Asili ya jinaKla. Ūranus, kutokana na Kgk. Οὐρᾰνός (Ouranós)
Alama♄
Tabia za njiamzingo
Umbali mfupikm 2,735,560,000
au 18.2861
Umbali mrefukm 3,006,390,000
au 20.0965
km 2,870,972,000
au 19.19126
Uduaradufu0.04717
siku 30,688.5
miaka 84.0205
Mwinamo0.773° toka njia ya Jua
Miezi27
Tabia za gimba
km 25,362±7
mara 3.976 ya Dunia
Tungamokg 8.6810×1025
mara 14.536 ya Dunia
g/cm3 1.27
Uvutano wa usoni
m/s2 8.69
Kasi ya kuponyokea
km/s 21.3
siku −0.71832
siku −0.71833
Weupe0.300 (Bond)
0.488 (jiometri)
HalijotoK 76 (−197.2°C)

Uranusi ni sayari ya saba kutoka Jua.

Asili ya jina

Waswahili wa kale hawakujua sayari hii. Uranusi ni jina la kimataifa lililoteuliwa katika karne ya 19 baada ya majadiliano marefu kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Ni jina la mungu wa Ugiriki ya Kale Urano (Kgi.Οὐρανός) aliyeaminiwa kuwa mungu wa anga. Lugha nyingi duniani zimepokea jina hili kwa sababu astronomia ya zamani haikujua sayari hii.

Vitabu kadhaa vinatumia jina la Kiswahili Zohali[1][2][3] kwa kufuata kamusi ya KAST; lakini hili ni jina la Kiswahili kwa sayari ya sita (Kng. Saturn).[4]

Tabia

Ni sayari kubwa ya tatu ya Mfumo wa Jua hata kama mada yake ni hasa gesi iliyoganda. Jumla ya masi yake ni mara 14 ya dunia hivyo ni sayari nyepesi kulingana na ukubwa wake. Kipenyo chake ni takriban kilomita 50,000[5].

Inazunguka Jua kwenye obiti inayochukua miaka 84. Umbali wake na Jua ni takriban mara 19 umbali wa Jua na Dunia au kilomita bilioni 2.9; afeli yake ni vizio astronomia 20.11 na periheli yake ni vizio astronomia 18.33.

Hadi mwaka 2023 miezi 27 iligunduliwa. Miezi mikubwa huitwa Miranda, Arieli, Umbrieli, Titania na Oberoni. Ina pia pete kadhaa yaani mawingu ya vumbi, barafu na mawe madogo ambayo ni nyembamba na kuzunguka sayari kwa umbo la pete. Pete za Uranusi ni hafifu kuliko zile za Zohali.

Uranusi inaonekana kama nyota hafifu sana yenye mwangaza wa 5.6 - 6. Kutokana na kuwa hafifu vile na mwendo wake wa pole hakuna utamaduni wowote wa kale ulioitambua kuwa sayari. Ilitambuliwa mara ya kwanza kuwa sayari na tarehe 13 Machi 1781 na William Herschel.

Tazama pia

Marejeo

  1. Wallah, W.B. & Mwamburi, J. Kiswahili mufti darasa la 8: Mwongozo wa mwalimu. Longhorn, 2009. ISBN 99966491066
  2. TESSA - Teacher Education in Sub Saharan Africa. Nishati na Mwendo: Kutoka Ardhini kenda kwenye nyota – kutumia Zana Kifani Archived 9 Aprili 2016 at the Wayback Machine.. Available at: www.tessafrica.net
  3. Waweru, M.; Makombo, H; Vonuoli, A.; Kashihiri, C.; Mwayani, J.Hutua za Kiswahili: Masomo ya Msingi 8. East African Educational Publishers ltd., 1ed, 290p., 2005. ISBN 9966-25-403-X
  4. KAST ni kamusi ya pekee inayotumia "Zohali" kwa sayari hii. Kamusi za KKK/ESD ya TUKI na M-J SES zinaonyesha "Zohali" kwa sayari ya sita na "Uranus" kwa sayari hii. Linganisha ukurasa wa Majadiliano:Sayari
  5. Uranus - by the numbers, tovuti ya NASA, iliangaliwa Januari 2021
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uranusi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoPasakaPasaka ya KikristoAlhamisi kuuAngkor WatOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoFasihi simuliziUbuntuOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaNgeli za nominoTanzaniaFasihiShairiIjumaa KuuMikoa ya TanzaniaLughaHomanyongo CJumuiya ya Afrika MasharikiKamusi za KiswahiliMofimuAina za manenoVivumishiModule:ArgumentsUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaSilabiNembo ya TanzaniaKiswahiliMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaDiamond PlatnumzOrodha ya makabila ya TanzaniaMaumivu ya kiunoOrodha ya Watakatifu WakristoKitenziDuniaKumaVitendawiliTamthiliaIndonesiaTafsiriNominoTendo la ndoaSentensiUandishi wa ripotiTanganyikaUwanja wa Taifa (Tanzania)Orodha ya nchi za AfrikaNguzo tano za UislamuHistoria ya KanisaNomino za pekeeYouTubeMuhammadHistoria ya KiswahiliJohn MagufuliVieleziBaike: Msaada wa kuanzisha makalaAmri KumiMaalum:MabadalikoyaKaribuniMbooWasukumaMshororoMawasilianoKisaweHafidh AmeirFasihi andishiTarakilishiDizasta VinaLigi ya Mabingwa AfrikaBendera ya TanzaniaSiku tatu kuu za PasakaSimba S.C.Young Africans S.C.UkimwiOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaOrodha ya Marais wa TanzaniaOrodha ya Magavana wa TanganyikaKiraiBaike: AboutOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaTashdidiKitenzi kishirikishiStadi za lughaAsili ya KiswahiliJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaRamaniHistoria ya AfrikaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniWilaya za TanzaniaMisimu (lugha)WachaggaMfumo wa JuaAgano la KaleKamusi ya Kiswahili sanifuMziziKwaresimaNomino za dhahaniaKamusiTabianchiAlama ya uakifishaji