Data

Data (wingi wa neno la Kilatini "Datum", ambayo kutumika kwa nadra) inamaanisha makundi ya habari. Data kwa kawaida ni matokeo ya vipimo na inaweza kuwa msingi wa jedwali, picha, au uchunguzi wa seti ya variables. Mara nyingi data huchukuliwa kama kiwango cha chini kabisa kwa ujumla ambapo habari na maarifa yaweza kutolewa.

Asili ya nenohariri

Neno "Datum" inamaanisha "kutoa", kwa hiyo inaweza kumaanisha "kitu kutolewa". Participle ya "kutoa" imetumiwa kwa muda wa milenia, kama taarifa iliyokubaliwa katika mijadala juu ya masuala ya jeometri, hisabati, uhandisi, na kadhalika. Pia, data huwakilisha matukio, takwimu, na wazo. Matumizi kama haya ndiyo asili ya data kama dhana katika sayansi ya tarakilishi au kompyuta ukipenda: data ni idadi, maneno, picha, n.k.: haya yote yanakubaliwa kama data.

Raw data kwa lugha ya Kiingereza ni mkusanyo wa idadi, picha au matokeo mengine kutoka kwa vifaa ili kuvibadilisha kuwa ishara, ambazo bado hazijasindikwa. Data hizo kwa kawaida hupitia usindikaji zaidi kwa binadamu au huingizwa katika kompyuta, huhifadhiwa na hupitia usindikaji huko, au hupelekwa (matokeo) kwa binadamu mwingine au kompyuta nyingine (kutumia waya). Raw data ni jina ambalo hubadilika; usindikaji wa data kwa kawaida hutokea hatua kwa hatua, na "data iliyosindikwa" kutoka hatua moja inaweza kuonekana kama "data ambayo haijasindikwa" (raw data) katika hatua ijayo.

Vifaa vya tarakilishi vya muwasho vimewekwa katika vikundi kulingana na njia ambazo zinawakilisha data. Tarakilishi ya aina ya "Analojia" inawakilisha Datum kama umbali au pozisheni. Tarakilishi ya aina ya "Digitali" inawakilisha Datum kama mlolongo wa ishara inayotolewa kutoka alfabeti isiyobadiliki. Tarakilishi za aina ya "Digital" zinazotumika sanasana hutumia alfabeti ya "binary", ambazo kwa kawaida ni namba "0" na "1". Aina tofauti za uwakilishaji zinazojulikana sana, kama vile idadi au alfabeti, vinajengwa kutoka kwa alfabeti ya "binary".

Baadhi ya fomu maalum ya data huwa ni tofauti. Programu ya kompyuta ni mkusanyo wa data, ambayo inaweza kufasiriwa kama maelekezo. Baadhi ya lugha za kompyuta hubainisha kati ya program ya kompyuta na data nyinginezo ambazo huendesha programu za kompyuta, lakini katika baadhi ya lugha za kompyuta, hasa Lisp na lugha zinazofanana, programu haziwezi kutofautishwa kimsingi kutoka data nyinginezo. Ni muhimu pia kutofautisha metadata, ambayo ni maelezo ya data nyinginezo. Jina lenye maana sawa na metadata lakini la kitambo ni "ancillary data". Mfano wa metadata ni maktaba ya katalogi, ambayo ni maelezo ya yaliyomo vitabuni.

Data ya majaribio inahusu data iliyotengenezwa katika muktadha wa uchunguzi wa kisayansi kupitia kutazama au kuchunguza na kurekodi.

Maana ya data, taarifa na maarifahariri

Maneno taarifa na maarifa mara nyingi hutumika katika dhana zinazobadilika. Tofauti kuu ni katika kiwango cha ujumla inayozingatiwa. Data iko katika ngazi ya chini, taarifa ni ngazi ya pili, na hatimaye, maarifa ni ngazi ya juu kati ya zote tatu. Data, kibinafsi haina maana yoyote. Ili data ibadilishwa kuwa taarifa, ni lazima data itafsiriwe na kupatiwa maana. Kwa mfano, urefu wa Mlima Everest kwa ujumla inachukuliwa kama "data", kitabu kuhusu sifa za Mlima Everest unaonekan kama “taarifa” na ripoti zenye taarifa kuhusu njia bora ya kufikia kilele cha Mlima Everest inaweza kuchukuliwa kama "maarifa".

Taarifa kama dhana huleta maana tofauti, kutoka kwa matumizi ya kila siku hadi mipangilio za kiufundi. Tukizungumza kwa ujumla, dhana ya taarifa inahusiana kwa karibu na wazo za vikwazo, mawasiliano, kudhibiti, data, umbo, mafundisho, maarifa, maana, kichocheo cha kiakili, muundo, mtazamo, na uwakilishi.

Beynon-Davies hutumia dhana ya ishara kutofautisha kati ya data na taarifa; data ni ishara ilhali taarifa hutokea wakati ishara zinatumiwa kumaanisha kitu fulani.[1][2]

Ni watu na kompyuta ambao hukusanya data na kulazimisha ruwaza kwa data. Ruwaza hizi ni huonekana kama taarifa ambayo inaweza kutumika kuongeza maarifa. Ruwaza hizi zinaweza kutafsiriwa kama ukweli, na zina mamlaka kama estetiska na vigezo vya kimaadili. Matukio ambayo huacha nyuma mabaki yanaweza kufikiwa data. Alama hazifikiriwi tena kama data mara tu kiungo kinachounganisha alama na mtazamo kinavunjwa. Hii inamaanisha kuwa, wakati tukio linawacha alama za habari, alama hizo zinapata hadhi ya data. [3]

Angalia Piahariri

Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
  • Data ya biolojia
  • Ununuzi wa data
  • Uchambuzi wa data
  • Waya ya data
  • Data domain
  • Data element
  • Data farming
  • Utawala wa data
  • Uadilifu wa data
  • Matengenezo ya data
  • Usimamizi wa data
  • Data mining
  • Data modeling
  • Usindikaji wa data ya kompyuta
  • Ahueni ya data
  • Data remanence
  • Seti ya data
  • Data warehouse
  • Database
  • Datasheet
  • Environmental data rescue
  • Metadata
  • Scientific data archiving
  • Takwimu
  • Datastructur

Marejeohariri

  1. P. Beynon-Davies (2002). Information Systems: An introduction to informatics in organisations. Basingstoke, UK: Palgrave. ISBN 0-333-96390-3. 
  2. P. Beynon-Davies (2009). Business information systems. Basingstoke, UK: Palgrave. ISBN 978-0-230-20368-6. 
  3. Sharon Daniel. The Database: An Aesthetics of Dignity. 

Viungo vya njehariri

🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoPasakaPasaka ya KikristoAlhamisi kuuAngkor WatOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoFasihi simuliziUbuntuOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaNgeli za nominoTanzaniaFasihiShairiIjumaa KuuMikoa ya TanzaniaLughaHomanyongo CJumuiya ya Afrika MasharikiKamusi za KiswahiliMofimuAina za manenoVivumishiModule:ArgumentsUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaSilabiNembo ya TanzaniaKiswahiliMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaDiamond PlatnumzOrodha ya makabila ya TanzaniaMaumivu ya kiunoOrodha ya Watakatifu WakristoKitenziDuniaKumaVitendawiliTamthiliaIndonesiaTafsiriNominoTendo la ndoaSentensiUandishi wa ripotiTanganyikaUwanja wa Taifa (Tanzania)Orodha ya nchi za AfrikaNguzo tano za UislamuHistoria ya KanisaNomino za pekeeYouTubeMuhammadHistoria ya KiswahiliJohn MagufuliVieleziBaike: Msaada wa kuanzisha makalaAmri KumiMaalum:MabadalikoyaKaribuniMbooWasukumaMshororoMawasilianoKisaweHafidh AmeirFasihi andishiTarakilishiDizasta VinaLigi ya Mabingwa AfrikaBendera ya TanzaniaSiku tatu kuu za PasakaSimba S.C.Young Africans S.C.UkimwiOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaOrodha ya Marais wa TanzaniaOrodha ya Magavana wa TanganyikaKiraiBaike: AboutOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaTashdidiKitenzi kishirikishiStadi za lughaAsili ya KiswahiliJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaRamaniHistoria ya AfrikaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniWilaya za TanzaniaMisimu (lugha)WachaggaMfumo wa JuaAgano la KaleKamusi ya Kiswahili sanifuMziziKwaresimaNomino za dhahaniaKamusiTabianchiAlama ya uakifishaji