Chad


Chad, kirasmi Jamhuri ya Chad (pia: Chadi), ni nchi huru iliyoko Afrika ya Kati. Imepakana na Libya, Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kamerun, Nigeria na Niger.

Jamhuri ya Chad
جمهورية تشاد (Kiarabu)
République du Tchad (Kifaransa)
Bendera ya Chad
Bendera
Nembo ya Chad
Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Unité, Travail, Progrès (Kifaransa)
الاتحاد، العمل، التقدم (Kiarabu)
"Umoja, Kazi, Maendeleo"
Wimbo wa taifa:
La Tchadienne (Kifaransa)
نشيد تشاد الوطني (Kiarabu)
"Wimbo wa Chad"
Mahali pa Chad
Mahali pa Chad
Ramani ya Chad
Ramani ya Chad
Mji mkuu
na mkubwa nchini
N'Djamena
12°06′ N 16°02′ E
Lugha rasmiKiarabu
Kifaransa
Makabila (asilimia)[1]26.6 Wasara
12.9 Waarabu
8.5 Wakanembu
7.2 Wamasalit
6.9 Watebu
4.8 Wamasana
3.7 Wabidiyo
3.7 Wabilala
3.0 Wamaba
2.6 Wadaju
2.5 Wamundang
2.4 Wagabri
2.4 Wazaghawa
2.1 Wafulani
2.0 Watupuri
1.6 Watama
1.4 Wakaro
1.3 Wabagirmi
1.0 Wamasmaje
2.6 Wachad wengine
0.7 Wageni
Dini (asilimia)[2]55.1 Waislamu
41.1 Wakristo
2.4 Wakanamungu
1.3 dini asilia
0.1 wengine
SerikaliJamhuri yenye
baraza la majeshi
 • Rais wa muda
 • Makamu wa Rais
 • Waziri Mkuu
Mahamat Déby
Djimadoum Tiraina
Succès Masra
Eneo
 • Eneo la jumlakm2 1 284 000[3]
 • Maji (asilimia)1.9[3]
Idadi ya watu
 • Kadirio la 202318 523 165[3]
Pato la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 12.596[4]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 702[4]
Pato halisi la taifaKadirio la 2023
 • JumlaOngezeko USD bilioni 32.375[4]
 • Kwa kila mtuOngezeko USD 1 806[4]
Maendeleo (2022)Ongezeko 0.394[5] - duni

Mji mkuu ni Ndjamena.

Jiografiahariri

Sehemu kubwa ya eneo lake ni jangwa na nchi yabisi. Kusini kuna kanda lenye hali ya hewa ya kitropiki, lakini ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo ni asilimia 3 tu za eneo lake lote .

Kaskazini kuna milima ya Tibesti.

Katikati liko beseni la ziwa Chad lililokuwa kati ya maziwa makubwa kabisa duniani lakini limepungua sana, hasa mwishoni mwa karne ya 20.

Historiahariri

Makala kuu: Historia ya Chad

Katika milenia ya 7 KK kulikuwa na watu wengi sana katika beseni hiyo.

Katika historia kabla ya ukoloni watu wa kaskazini waliwafanyia vita watu wa kusini na kuteka wafungwa kama watumwa. Hivyo hadi leo uhusiano kati ya kusini na kaskazini ya nchi ni mgumu.

Tangu mwaka 2003 petroli imekuwa inaongoza kati ya bidhaa zinazopelekwa nje ya nchi badala ya pamba.

Tangu mwaka huo Mgogoro wa Darfur nchini Sudan umevuka mpaka na kuvuruga Chad pia. Ikiwa kati ya nchi zinazoongoza duniani kwa ufukara na ufisadi, ilipata shida kupokea wakimbizi kwa mamia elfu.

Ingawa kulikuwa na vyama vingi vya siasa na mapigano ya kisiasa pamoja na majaribio ya mapinduzi, mamlaka ilibaki imara mikononi mwa Rais Déby na chama chake, Patriotic Salvation Movement, hadi alipouawa mwaka 2021.

Watuhariri

Msichana wa mkoa wa Ouaddaï.

Wakazi walikuwa 15,500,000 mwaka 2018.

Jinsi ilivyo katika nchi mbalimbali za kanda la Sahel kuna aina mbili za wakazi ndani yake:

Kwa jumla leo kuna makabila zaidi ya 200 nchini, ambayo hutimia lugha na lahaja zaidi ya 100 (angalia orodha ya lugha hizo). Asili yao ni Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi na Afrika Kaskazini vilevile[9].

Lugha rasmi ni Kiarabu na Kifaransa.

Tazama piahariri

Marejeohariri

  1. Analyse Thematique des Resultats Definitifs Etat et Structures de la Population. Institut National de la Statistique, des Études Économiques et Démographiques du Tchad. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-12-28. Iliwekwa mnamo 2024-03-27.
  2. Religions in Chad | PEW-GRF.
  3. 3.0 3.1 3.2 Chad. The World Factbook. Central Intelligence Agency.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Chad). International Monetary Fund (10 October 2023).
  5. Human Development Report 2023/24 (en). United Nations Development Programme (13 March 2024).
  6. Table: Muslim Population by Country. Pew Research Center. Iliwekwa mnamo 16 April 2018.
  7. The World's Muslims: Unity and Diversity 128–129. Pew Forum on Religious & Public life (9 August 2012). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-10-24. Iliwekwa mnamo 2 June 2014.
  8. Table: Christian Population as Percentages of Total Population by Country. Pew Research Center. Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-05-11. Iliwekwa mnamo 16 April 2018.
  9. Haber, Marc; Mezzavilla, Massimo; Bergström, Anders; Prado-Martinez, Javier; Hallast, Pille; Saif-Ali, Riyadh; Al-Habori, Molham; Dedoussis, George; Zeggini, Eleftheria; Blue-Smith, Jason; Wells, R. Spencer; Xue, Yali; Zalloua, Pierre A.; Tyler-Smith, Chris (1 December 2016). "Chad Genetic Diversity Reveals an African History Marked by Multiple Holocene Eurasian Migrations". The American Journal of Human Genetics (in English) 99 (6): 1316–1324. ISSN 0002-9297. PMC 5142112 Check |pmc= value (help). PMID 27889059. doi:10.1016/j.ajhg.2016.10.012. 

Marejeo menginehariri

Viungo vya njehariri

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Vya serikali
Vingine


Nchi za Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Chad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Chad Country Commercial Guide – FY 2005". Jalada kutoka ya awali juu ya 2007-10-15. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.. United States Department of Commerce.
🔥 Top keywords: Maalum:TafutaMwanzoPasakaPasaka ya KikristoAlhamisi kuuAngkor WatOrodha ya mikoa ya Tanzania kwa eneoFasihi simuliziUbuntuOrodha ya Mawaziri Wakuu wa TanzaniaNgeli za nominoTanzaniaFasihiShairiIjumaa KuuMikoa ya TanzaniaLughaHomanyongo CJumuiya ya Afrika MasharikiKamusi za KiswahiliMofimuAina za manenoVivumishiModule:ArgumentsUfahamu wa uwezo wa kushika mimbaSilabiNembo ya TanzaniaKiswahiliMfumo wa mmeng'enyo wa chakulaDiamond PlatnumzOrodha ya makabila ya TanzaniaMaumivu ya kiunoOrodha ya Watakatifu WakristoKitenziDuniaKumaVitendawiliTamthiliaIndonesiaTafsiriNominoTendo la ndoaSentensiUandishi wa ripotiTanganyikaUwanja wa Taifa (Tanzania)Orodha ya nchi za AfrikaNguzo tano za UislamuHistoria ya KanisaNomino za pekeeYouTubeMuhammadHistoria ya KiswahiliJohn MagufuliVieleziBaike: Msaada wa kuanzisha makalaAmri KumiMaalum:MabadalikoyaKaribuniMbooWasukumaMshororoMawasilianoKisaweHafidh AmeirFasihi andishiTarakilishiDizasta VinaLigi ya Mabingwa AfrikaBendera ya TanzaniaSiku tatu kuu za PasakaSimba S.C.Young Africans S.C.UkimwiOrodha ya Makamu wa Rais TanzaniaOrodha ya Marais wa TanzaniaOrodha ya Magavana wa TanganyikaKiraiBaike: AboutOrodha ya Maspika wa Bunge la TanzaniaTashdidiKitenzi kishirikishiStadi za lughaAsili ya KiswahiliJumuiya ya Maendeleo Kusini mwa AfrikaRamaniHistoria ya AfrikaAfrika ya Mashariki ya KijerumaniWilaya za TanzaniaMisimu (lugha)WachaggaMfumo wa JuaAgano la KaleKamusi ya Kiswahili sanifuMziziKwaresimaNomino za dhahaniaKamusiTabianchiAlama ya uakifishaji